Chelsea Yajipigia Westham Mkono

Klabu ya Chelsea imetakata ikiwa katika dimba lao la Stamford Bridge baada ya kuibamiza klabu ya Westham United kwa jumla ya mabao matano kwa bila katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza.

Chelsea inafanikiwa kushinda katika uwanja wao wa nyumbani mfululizo baada ya kuipiga klabu ya Tottenham katikati ya wiki, Leo tena wamefanikiwa kuifunga klabu ya Westham tena kwa kipigo kikubwa.chelseaMatajiri hao wa jiji la London walionekana kutawala mchezo kuanzia dakika ya kwanza kwani walifanikiwa kutengeneza nafasi za magoli kadhaa ndani ya kipindi cha kwanza na kufanikiwa kupata mabao matatu kupitia kwa Cole Palmer, Conar Gallagher, na Noni Madueke.

Kipindi cha pili vijana wa kocha Pochettino walionekana kuendelea kua na njaa kwani walifanikiwa kufunga mabao mengine mawili kupitia kwa mshambuliaji wao Nicklas Jackson ambaye alifanikiwa kufunga mabao mawili na kukamilisha ushindi wa kibabe kabisa.chelseaBaada ya klabu ya Chelsea kufanikiwa kupata ushindi huo sasa wamefanikiwa kufikisha jumla ya alama 54 na kufanikiwa kupanda mpaka nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, Huku wakifanikiwa kuishusha klabu ya Man United ambayo imeshuka mpaka nafasi ya nane.

Acha ujumbe