Chelsea Majanga Matupu

Klabu ya Chelsea imeendelea kuandamwa na majanga kwani wachezaji wake muhimu wanaendelea kupata majeraha ambapo wachezaji wawili wa klabu hiyo wamepata majeraha tena.

Kiungo Enzo Fernandez na beki Axel Disasi wameripotiwa kupata majeraha na kuongeza orodha ya wachezaji majeruhi ndani ya klabu ya Chelsea jambo ambalo linaendelea kuonesha klabu hiyo ipo kwenye wakati mgumu.chelseaMatajiri hao wa jiji la London wamekua kwenye kipindi kigumu sana msimu huu na sababu mojawapo ni klabu hiyo kuandamwa na majeraha haswa wachezaji wanaounda kikosi cha kwanza cha klabu hiyo.

Mpaka sasa klabu ya Chelsea imekua na wachezaji takribani tisa wa kikosi cha kwanza walio majeraha na hii orodha imekuja baada ya kuongezeka kwa Axel Disasi na kiungo anayefanya vizuri klabuni hapo Enzo Fernandez.chelseaMpaka sasa wachezaji ambao wapo majeruhi klabuni hapo ni Reece James, Levi Colwill, Raheem Sterling, Romeo Lavia, Wesley Fofana, Christopher Nkunku, pamoja na golikipa Robert Sanchez wakati huo wameongezeka wawili kutokana na taarifa iliyotoka mapema leo.

Acha ujumbe