Kiungo wa Klabu ya Yanga Pacome Zouzoua amefunguka siku ambayo atarejea Uwanjani, Baada ya kukosekana Kwa muda mrefu.
Hadi kufikia leo, inakuwa zimefika takribani wiki nne tangu alipopata jeraha kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.
Alizungumzia Maendeleo ya Afya yake, Pacome alisema, anashukuru Mungu kuwa Kila kitu kinakwenda sawa kuhusu Afya yake na muda wowote atakuwa tayari kurudi Uwanjani kuipambania timu yake.
“Namshukuru Mungu, Baada ya kupita takribani mwezi mmoja Sasa nikiwa nje ya uwanja, nimeanza kurejea kwenye utimamu wangu.”
Nadhani siku siyo nyingi nitakuwa tayari kurejea Uwanjani Kwa kuwa nimekuwa nikiingia taratibu kwenye mazoezi ya pamoja na wenzangu, alisema PACOME.