Kocha wa klabu ya Barcelona Xavi Hernandez kwenye hali ya kushangaza amewashtua mashabiki wa klabu hiyo baada ya kutangazwa kua ataendelea kusalia ndani ya viunga vya klabu hiyo vya Camp Nou.
Kocha Xavi alitangazwa kua ataondoka ndani ya klabu hiyo baada ya kumalizika kwa msimu huu, Lakini taarifa zimekua za tofauti kwani kocha huyo amebadili msimamo wake na ataendelea kukionoa kikosi cha Blaugrana msimu ujao.Taarifa zilieleza mwanzo kua klabu ya Barcelona inafanya mazungumzo na makocha mbalimbali kwajili kuchukua mikoba ya Xavi, Lakini taarifa za kushangaza ni kua klabu hiyo kupitia raia wake inaeleza haikuwahi kufanya mazungumzo na kocha yeyote.
Rais wa Barcelona Joan Laporta amesema hawakuwahi kufanya mazungumzo na kocha yeyote wakati kocha huyo ametangaza kuondoka klabuni hapo, Kwani wao walikua wanasubiriwa kiungo huyo wa zamani wa klabu hiyo abadili maamuzi yake kwani walikua wakimsisitiza kufanya hivo.Kocha Xavi amekua hana wakati mzuri sana ndani ya Barcelona msimu huu lakini msimu uliomalizika alifanikiwa kuipatia klabu hiyo taji la ligi kuu ya Hispania, Hivo klabu hiyo inaamini kocha huyo bado anaweza kuirudisha klabu hiyo kwenye zama zake za mafanikio.