Michael Olise Kwenye Rada za United

Winga wa klabu ya Crystal Palace raia wa kimataifa wa Ufaransa Michael Olise yupo kwenye rada za klabu ya Manchester United kuelekea dirisha kubwa la usajili mwezi Julai mwaka huu.

MichaelOlise anaelezwa kufuatiliwa kwa karibu na Man United kuliko mchezaji mwingine yeyote kuelekea dirisha hili kubwa, Huku gharama ya usajili ya mchezaji huyo ikikadiriwa kama kiasi cha paundi milioni 60.michael oliseVilabu vingine vinaelezwa kumfuatilia pia mchezaji huyo ila mashetani wekundu ndio wanaongoza katika mbio hizo, Kwani mchezaji huyo amekua kwenye rada za klabu hiyo tangu dirisha dogo la mwezi Januari.

Manchester United inaingia sokoni kwa nguvu kubwa kwajili ya kuhakikisha wanakijenga kikosi chao ili kuweza kugombania mataji msimu ujao, Kwani msimu huu wamekua na msimu mbaya sana jambo ambalo viongozi wa klabu hiyo hawataki lijirudie.michael oliseWinga Michael Olise anaweza kua usajili wa kwanza wa klabu ya Man United kama kila kitu kitaenda sawa, Kwani ni moja ya wachezaji ambao wanafuatiliwa kwa karibu zaidi na klabu ya Manchester United kwajili ya kukiboresha kikosi hicho na mchezaji huyo amefuatiliwa kwa karibu na klabu hiyo kwa muda na wamejiridhisha ubora wake.

 

Acha ujumbe