Borussia Dortmund Wana Mpango wa Kumbakiza Sancho

Klabu ya Borussia Dortmund kupitia kwa mkurugenzi wa klabu hiyo Sebastian Kehl ameeleza mpango wao ni kutaka kumbakiza winga Jadon Sancho anayekipiga klabuni hapo kwa mkopo akitokea Man United Jadon Sancho.

Borussia Dortmund wameweka wazi kua watafanya kila namna kuhakikisha wanambakiza winga Jadon Sancho, Kwani winga huyo amekua kwenye ubora mkubwa sana tangu arejee klabuni hapo mwezi Januari mwaka huu.borussia dortmundMkurugenzi Sebastian Kehl anaeleza mpango wao ni kumbakiza Sancho lakini itategemea pia na klabu ya Manchester United ambao ndio wamiliki halali wa mchezaji huyo watakua wana mpango gani juu ya mchezaji huyo.

Mkurugenzi huyo amesema Man United wameona kwa namna ambayo Sancho amekua akicheza vizuri kwasasa, Hivo wanaweza kufikria kumuuza kwa ofa nzuri au kumrejesha ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.borussia dortmundSancho amekua akifanya vizuri tangu arejee Borussia Dortmund kwa mkopo jambo ambalo limewafanya mabosi wa klabu hiyo kuhitaji kumbakiza ndani ya timu hiyo,Huku Man United wanaelezwa wako tayari kumuuza mchezaji huyo lakini kwa ofa nzuri.

Acha ujumbe