Kocha wa klabu ya soka ya Chelsea Mauricio Pochettino ameoneshwa kuchukizwa na maswali ya hatma yake ndani ya klabu hiyo na kua huenda akaondoka ndani ya timu hiyo mwishoni mwa msimu.
Kocha Pochettino bado ana mkataba wa mwaka mmoja ndani ya klabu hiyo hivo maswali ambayo anaulizwa kuhusu kuondoka kwake hayampendezi, Huku kwasasa akiwaambia wanahabari wanapaswa kuiuliza klabu juu ya hatma yake na sio yeye.Mpaka sasa kocha huyo anaamini ataendelea kuwepo ndani ya klabu hiyo msimu ujao kwakua bado ana mkataba ndani ya klabu hiyo tajiri kutoka jiji la London, Huku akieleza kama kutakua na maamuzi mengine yataonekana ila kwasasa bado yupo ndani ya klabu hiyo
Klabu ya Chelsea imekua kwenye kipindi kigumu msimu huu huku baada ya ushindi wa jana dhidi ya Tottenham wa mabao mawili kwa bila ukiwapeleka nafasi ya nane kwenye ikiwa ndio nafasi yao ya juu zaidi msimu huu, Kupitia wakati mgumu kwa klabu hiyo ndio kunapelekea kocha huyo kuhusishwa kutimka mara kwa mara.Klabu ya Chelsea pia wamekua wakihusishwa na makocha kadhaa kuelekea msimu kumalizika hii ikiwa sio ishara nzuri kwa kocha Pochettino, Lakini kocha huyo ameonesha kujiamini na kuwaeleza wanahabari kua bado yupo klabuni hapo na kama kutatokea chochote cha tofauti yeye yupo tayari.