Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag leo amefunguka kua ni kweli alimuhitaji kiungo wa klabu ya Barcelona aje klabuni hapo pamoja na kiungo Carlos Casemiro kutoka klabu ya Real Madrid.
Mwaka 2022 kwenye dirisha kubwa la usajili klabu ya Manchester United ilihusishwa kwa kiwango kikubwa na kiungo wa klabu ya Fc Barcelona Frenkie De Jong japokua hawakumpata mpaka dirisha linafungwa.Kocha Ten Hag akifanya mazungumzo kwenye kipindi kimoja nchini Uingereza na gwiji wa zamani wa klabu hiyo Gary Neville amefunguka na kusema” Ni kweli mwaka 2022 nilimuhitaji De Jong pamoja na Casemiro kwa pamoja kwakua wangesaidiana vizuri, Lakini hatukufanikiwa kuwapata wote na sio kila mchezaji unaemtaka utampata na unapaswa kukubali hilo”
Taarifa nyingi zimekua zikieleza kua kiungo Casemiro alisajiliwa ndani ya Man United kama mbadala wa Frenkie de Jong ambaye alikosekana, Lakini kocha huyo ameweka wazi Casemiro hakusajiliwa kwakua usajili wa Frenkie ulifeli bali ulikua mpango kuwasajili wote kwa pamoja.Kocha Ten Hag wakati akifanya mahojiano hayo mbali na usajili wa Frenkie de Jong aliweza kugusia pia juu ya kumuhitaji mshambuliaji Harry Kane anayekipiga ndani ya klabu ya bayern Munich kwasasa, Lakini hakufanikiwa kumpata pia mchezaji huyo kwenye majira ya joto yaliyopita.