AHMED ALLY: SIMBA NDO TIMU YENYE WACHEZAJI BORA ZAIDI

MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally, ametoa kauli ya kibabe, akisema timu ndiyo yenye wachezaji bora kuliko timu yoyote nchi hii.

Kauli hiyo inakuja baada ya uvumi wa taarifa nyingi zikidai baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wanawindwa na klabu nyingi za nje na ndani ya Tanzania.AHMED ALLY“Licha ya timu yetu kusemekana ni mbovu lakini ndio timu inayoongoza kwa wachezaji wake kuhitajika na vilabu vingi zaidi vya ndani na nje nchi.

Alisema Ahmed Ally”Ni dhahiri kuwa tuna kikosi chenye Wachezaji bora.

“Hatujapata matokeo mazuri msimu huu lakini haindoi ukweli kuwa wachezaji wetu ni bora sana ndio maana wanatajwa sana sokoni.

“Tunachoenda kukifanya hivi sasa ni kubaki na wale bora wenye moyo wa kuitumikia Simba. Alisema Ahmed Ally

 

AHMED ALLY

 

 

“Katika dirisha hili la usajili tunaemtaka atabaki Simba lengo ni kutengeneza Simba tishio turudi kwenye Ufalme wetu.”

Acha ujumbe