SIMBA SAFARI YA MATUMAINI ZANZIBAR

SIMBA wametinga hatua ya nusu fainali kwenye Mashindano ya Muungano Cup yaliyorejea Jana huko Visiwani Unguja, Zanzibar.

Mshambuliaji anayesemwa sana kuwa ni wa kawaida, Fred Michael ndiye aliyeweka kwenye kamba bao la kwanza mapema kipindi Cha kwanza, kabla la mlinzi Israh Mwenda hajafunga bao la ushindi.SIMBAMashindano hayo yanabaki kuwa tumaini lingine la Simba kuona kama wanaweza kumaliza Msimu wakiwa na Kombe mkononi, hiyo ni baada ya kuipoteza Kombe la FA na kuwa na matumaini dhaifu sana ya kuwa Bingwa wa NBC.

Kocha Msaidizi wa Simba Suleiman Matola amesema Wana Kila Sababu ya kuwa Mabingwa kwenye Mashindano hayo Ili kurejesha matumaini ya Wanasimba.SIMBA“Nadhani tuna Kila Sababu ya kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano haya, timu Haina mwenendo mzuri, lakini Haina maana tunaweza kufanya vibaya kwenye Kila mchezo,” alisema Matola.

Acha ujumbe