NDANI ya msimu wa 2023/24 yamekuwa ni mapito magumu kwa Mtibwa Sugar inayopambana kubaki ndani ya ligi kwa kusaka matokeo katika mechi zilizobaki.
Sio nyumbani wala ugenini hali haijawa nzuri katika kupata matokeo ndani ya dakika 90 uwanjani chini ya Kocha Mkuu, Zuber Katwila.
Aprili haijawa njema pia katika mashindano yake yote iligotea hatua ya 16 bora kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma Azam FC 3-0 Mtibwa Sugar.Aprili 13 ilikuwa mchezo wa Ligi Kuu Bara wakiwa Uwanja wa Manungu ulisoma Mtibwa Sugar 2-2 Geita Gold wakagawana pointi mojamoja .
Aprili 16 2024 ilikuwa Mtibwa Sugar 0-1 KMC katika mchezo huu bahati haikuwa kwa Mtibwa Sugar kwa kuwa walipata pigo la penalti ikaokolewa na KMC.
Funga Aprili ilikuwa ni Aprili 28 2024 ubao wa Meja Isamuhyo ulisoma JKT Tanzania 2-1 Mtibwa Sugar, kituo kinachofuata ni dhidi ya Simba ikiwa ni mzunguko wa pili