SIMBA KUIFUATA KAGERA KINYONGE

BAADA ya kugawana pointi mojamoja dhidi ya Namungo, Uwanja wa Majaliwa kete inayofuata kwa Simba ni dhidi ya Mtibwa Sugar.

Chini ya Kocha Mkuu Juma Mgunda akishirikiana na Seleman Matola mchezo wao wa kwanza kukaa benchi walishuhudia ubao ukisoma Namungo 2-2 Simba.SIMBATimu hiyo ndani ya tatu bora haijawa na mwendo mzuri na itamkosa kiungo Clatous Chama ambaye amefungiwa mechi tatu kwa kosa la kumchezea faulo makusudi beki wa Yanga, Nickson Kibabage katika Kariakoo Dabi.

Ikumbukwe kwamba Mtibwa Sugar mchezo wake uliopita ilipoteza pointi tatu kwa kushuhudia ubao ukisoma JKT Tanzania 2-1 Mtibwa Sugar.SIMBA

Ni Mei 3 2024 mchezo huo na unatarajiwa kuchezwa kwa kila timu kuoambania pointi tatu.

Acha ujumbe