Chelsea Kufuta Uteja kwa Man United Leo?

Klabu ya Chelsea itaweza kufuta uteja kwa klabu ya Manchester United leo katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza utakaopigwa usiku wa leo ndio kitendawili kikubwa kwa matajiri hao wa London leo.

Chelsea ambao wamekua wanyonge kwa klabu ya Manchester United haswa kwenye michezo ya ligi kuu ya Uingereza, Hivo mchezo wa leo unaweza kuwapa nafasi ya kujiuliza ama kufuta uteja mbele ya mashetani hao wekundu kutoka jiji la Manchester.chelseaManchester United haijapoteza mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Chelsea tangu mwezi Novemba mwaka 2027 walipopoteza kwa bao moja kwa bila katika dimba la Stamford Bridge, Hivo ni miaka takribani saba sasa hawafungwa mchezo wowote na klabu hiyo kutoka jiji la London.

Mchezo wa leo ni muhimu kwa vilabu vyote ambapo matajiri wa London watahitaji kushinda mchezo huu ili kufuta uteja wao mbele ya Mashetani wekundu, Lakini Man United wao watahitaji kushinda mchezo huo ili kuendelea kupambana kumaliza nafasi nne za juu.chelseaMatajiri wa jiji London klabu ya Chelsea historia inaweza ikawabeba leo kwani mara ya mwisho kuifunga Manchester United ilikua katika dimba lao la nyumbani la Stamford Bridge, Hivo wanaweza wakairudisha historia nyuma na kushinda leo katika uwanja wao nyumbani.

 

Acha ujumbe