Joao Felix Amtamani Bernardo Barcelona

Mchezaji wa klabu ya Atletico Madrid Joao Felix anayekipiga kwa mkopo klabu ya Barcelona ameonesha kutamani mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Ureno Bernardo Silva kujiunga na Barcelona.

Akifanya mazungumzo na chombo kimoja cha habari nchini Hispania Joao Felix amesema ana matumaini klabu ya Barcelona wataenda kumsajili Bernardo Silva anayekipiga klabu ya Manchester City kwasasa.joao felixWinga huyo amesema kua kiungo Bernardo Silva amekua akimuuliza mara kwa mara kuhusiana na Barcelona, Lakini akaongeza kua familia yake pia ipo ndani ya jiji hilo hivo anaamini klabu hiyo kutoka Catalan inapaswa kumsajili mchezaji huyo.

Winga huyo wa kimataifa wa Ureno Joao Felix anasema kiungo Bernardo Silva ni aina ya mchezaji ambaye anaweza kuendana na klabu ya Barcelona, Lakini pia akisisitiza mchezaji huyo ni moja wachezaji bora sana na ni mtu mzuri pia.joao felixMkataba wa Bernardo Silva unamalizika mwezi Juni mwaka 2026 ambapo alisaini mkataba dirisha kubwa lililopita, Lakini kuna kiwango cha pesa klabu yeyote itakayomtaka itaweza kumpata ikilipa kiasi hicho ambacho ni paundi milioni 50 ikumbukwe pia klabu ya Barcelona imekua ikimfukuzia kiungo huyo kwa muda mrefu.

Acha ujumbe