Ten Hag: Tunataka Kufuzu Ligi ya Mabingwa

Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag amesema anatamani kuiona klabu yake inafuzu kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ulaya msimu ujao licha ya kutokua kwenye nafasi nzuri kwasasa.

Kocha Ten Hag amesema “Tuko kwenye daraja la juu,Nitasikitika kama tutashindwa kufuzu ligi ya mabingwa ulaya msimu ujao”Haya ni maneno ya kocha huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wao dhidi ya klabu ya Chelsea leo.ten hagManchester United wanakamata nafasi ya sita katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza wakiwa na alama 48, Huku wakiachwa alama 9 na Tottenham walioko nafasi ya tano wenye alama 57 hii inaonesha ni kwa kiwango gani ni ngumu kwa klabu hiyo kufuzu ligi ya mabingwa ulaya.

Kocha Erik Ten Hag mwenyewe ameeleza anatambua ugumu ambao utakuepo kuweza kumaliza katika nafasi nne za juu, Lakini amesisitiza watahakikisha wanapambana kwa mpaka siku za mwisho ili kuweza kuipata nafasi hiyo.ten hagManchester United wamekua hawana msimu mzuri kwani msimu uliomalizika mpaka sasa walikua  ndani ya nafasi nne za juu, Lakini msimu hali inaonekana kua tofauti kwani wanapaswa kushinda michezo yao huku wakiombea vilabu kama Tottenham na Aston Villa wapoteze michezo yao.

Acha ujumbe