Ten Hag Akanusha Rashford Kutimka

Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag amekanusha taarifa za mshambuliaji wake klabuni hapo Marcus Rashford kuhusishwa na mabingwa wa ligi kuu ya Ufaransa klabu ya PSG.

Kumekua na tetesi ambazo zinaeleza kua klabu ya PSG imejiandaa kutuma ofa ya kumsajili mshambuliaji huyo raia wa kimataifa wa Uingereza, Jambo ambalo limemfanya kocha Ten Hag kukanusha taarifa hizo.ten hagKatika mkutano wa waandishi wa habari leo kocha huyo wa kimataifa wa Uholanzi alisema “Hatukumpa mkataba wa miaka minne Rashford mwaka jana kwasababu ya kuja kumuuza, Anapaswa kua kwenye mradi wa Man United na sio jambo la kuficha”

Marcus Rashford imekua mara ya pili kwa klabu ya PSG kuhusishwa na mchezaji huyo lakini bado haijaonekana kama ni jambo ambalo linaweza kuwezekana kwani Man United walimuongezea mkataba mchezaji huyo ikionesha yupo kwenye mipango yao ya muda mrefu.ten hagKlabu ya PSG inaelezwa inatafuta mbadala wa Kylian Mbappe ambaye ameshatangaza kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu, Hivo klabu hiyo inamuona Rashford kama mbadala sahihi lakini kocha Ten Hag ameweka wazi kua hawako tayari kumuachia mchezaji huyo.

Acha ujumbe