Droo ya ligi ya mabingwa ulaya imechezeshwa na moja ya timu zitakazokutana katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya, Huku moja ya michezo ni kati ya Real Madrid dhidi ya Manchester City.
Mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Manchester City utakua mchezo wa kisasi kwani klabu ya Real Madrid ilitolewa kwenye michuano huyo kwa aibu baada ya kufungwa mabao manne kwa bila katika dimba la Etihad.Vilabu hivi vinakwenda kukutana kwa mara ya tatu kwa ndani ya misimu mitatu mfululizo, Huku walipokutana mara ya mwisho ilikua katika hatua ya nusu fainali mara mbili ambapo nusu fainali ya kwanza 2022 Real Madrid walishinda na mwaka jana walishinda Man City.
Mchezo huu umekua na mvuto na wa kusisimua sana pindi vilabu hivi vinapokutana kutokana na ubora ambao vilabu hivi imekua navyo miaka ya hivi karibuni, Na mwaka huu wanakwenda kukutana tena ikiwa sio hatua ya nusu fainali awamu hii ni robo fainali.Mchezo huu utaanza kupigwa katika dimba la Santiago Bernabeu na mzunguko wa wa pili utapigwa katika dimba la Etihad, Hii itakua inajirudia kwani msimu uliomalizika mchezo ulianzia Bernabeu na kumalizikia Etihad tofauti mwaka huu ni robo fainali mwaka jana ilikua nusu fainali.