Chelsea Majeraha Yaendelea Kuwaandama

Klabu ya Chelsea imeendelea kuandamwa na majeraha katika kikosi chao haswa katika wachezaji ambao wanaunda kikosi cha kwanza cha klabu hiyo.

Beki wa kushoto wa klabu hiyo ambaye ni nahodha msaidizi klabu hapo Ben Chilwell baada ya kutoka kwenye majeraha hivi karibuni, Lakini amepata majeraha kwa mara nyingine tena huku timu ya madaktari ya klabu ya hiyo ikiendelea na uchunguzi zaidi.

Klabu ya Chelsea imekua moja ya vilabu ambavyo vimekubwa na majeraha sana msimu huu na kua moja ya changamoto zaidi ndani ya klabu hiyo, Beki huyo ameungana wachezaji kama Reece James, Romeo Lavia, Levi Colwill pamoja na Christopher Nkunku.chelseaBeki huyo amekua akiandamwa na majeraha mara kwa mara ndani ya timu hiyo akiungana na nahodha namba moja wa timu hiyo Reece James, Jambo ambalo limekua likiisumbua klabu ya Chelsea kwani wachezaji ambao wanapata majeraha sana ndani ya timu ni wachezaji muhimu sana.

Acha ujumbe