Liverpool Yapigwa Tena Nyumbani

Klabu ya Liverpool imeendela ilipoishia katikati ya wiki na hiyo ni baada ya kukubali kipigo cha goli moja kwa bila leo katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Crystal Palace wakiwa nyumbani.

Liverpool wamekua na wiki ngumu sana kwani katikati ya wiki walipoteza nyumbani kwa mabao matatu kwa bila dhidi ya klabu ya Atalanta katika mchezo wa Uefa Europa League, Lakini wamepokea kipigo kingine mbele ya Palace katika uwanja wao nyumbani tena kwa goli la mapema kutoka kwa kiungo Eberechi Eze.liverpoolMajogoo hao wa Anfield sasa wamecheza mchezo wao wa tatu bila kushinda mchezo wowote kwani wikiendi iliyomalizika walipata sare dhidi ya Man United, Huku michezo miwili yote iliyofata wamepokea kichapo ikiwaweka kwenye mazingira mabaya katika mbio za ubingwa.

Matokeo ya leo yanawaacha Liverpool kwenye wakati mgumu katika mbio za ubingwa baada ya kutoka nafasi ya kwanza wakashuka nafasi ya pili, Leo sasa wanashuka mpaka nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.liverpoolKlabu ya Arsenal kama watafanikiwa kushinda mchezo wao wa leo dhidi ya Aston Villa watarejea kileleni kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, Huku Man City wakikamata nafasi ya pili na vijana wa Jurgen Klopp wakishuka mpaka nafasi ya tatu huku wakiachwa kwa alama tatu na vinara Arsenal.

Acha ujumbe