Kocha wa klabu ya Newcastle United Eddie Howe ameweka wazi kua hawana mpango wa kumuachia mshambuliaji wao kinara ndani ya timu hiyo Alexender Isak kwenda timu nyingine.
Kocha Eddie Howe ameamua kufunguka kutokana na tetesi mbalimbali ambazo zimekua zikimuhusisha Isak kutimka ndani ya klabu hiyo, Kwani amekua akihusishwa na vilabu kadhaa ndani ya ligi kuu ya Uingereza.Kocha huyo raia wa kimataifa wa Uingereza alisema “Tunajaribu kutengeneza timu hapa hivo tunahitaji kuwabakiza wachezaji wetu bora” Kauli hii inakuonesha klabu ya Newcastle hawafikirii kumuachia mshambuliaji Isak kwasasa.
Klabu ya Newcastle wapo kwenye mchakato wa kuhakikisha wanarudi kwenye ubora ambao walikua nao miaka mingi iliyopita, Hivo sio jambo jepesi kumuachia mchezaji ambaye anafanya vizuri ndani ya timu hiyo na akiibeba katika michezo mingi msimu huu.Mshambuliaji Alexender Isak amekua na msimu bora sana jambo limemfanya kuanza kufuatiliwa na vilabu kadhaa vikubwa nchini Uingereza, Lakini kocha Eddie Howe anaweka wazi hakuna namna wanaweza kukubali kumuachia mshambuliaji huyo hatari klabuni hapo.