Bayern Leverkusen Mabingwa Wapya Bundesliga

Klabu ya Bayern Leverkusen imefanikia kutwaa taji la Bundesliga baada ya kufanikiwa kupata ushindi mnono wa mabao matano kwa bila mbele ya klabu ya Weder Bremen.

Bayern Leverkusen wanatwaa ubingwa Bundesliga baada ya utawala wa muda mrefu wa klabu ya Fc Bayern Munich ambao wamebeba ubingwa huo mara 11 mfululizo lakini vijana wa Xabi Alonso wamevunja rekosi hiyo msimu huu.bayern leverkusenKlabu hiyo ambayo leo ilikua katika uwanja wake wa nyumbani na kufanikiwa kushusha kipigo kizito kwa klabu ya Weder Bremen,Ikumbukwe mbali na kutwaa ubingwa lakini pia klabu hiyo ndio inatwaa ubingwa wake wa kwanza wa Bundesliga katika historia ya klabu hiyo.

Mabao matatu ya kijana mdogo Florian Wirtz, Granit Xhaka na Victor Boniface yalitosha kabisa kuhakikisha klabu hiyo inatwaa ubingwa wa ligi kuu ya  Ujerumani huku ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja kwenye ligi hiyo mpaka sasa.

Vijana wa Xabi Alonso wanatwaa ubingwa wa ligi kuu ya Ujerumani wakiwa wamecheza michezo 29 wakiwa na michezo mitano mkononi, rekodi ambayo wanaitafuta klabu hiyo kwasasa ni kumaliza michezo yao bila kufungwa kwani wameshafanikiwa kutwaa ubingwa.bayern leverkusenKocha wa klabu hiyo Xabi Alonso amekua na wakati mzuri sana ndani ya timu hiyo tangu ameichukua timu hiyo mwaka jana, Kwani amefanikiwa kutengeneza timu hiyo kua moja ya timu tishio barani ulaya lakini pia kuwapa Bayern Leverkusen taji lao la kwanza la Bundesliga katika historia ya klabu hiyo kocha huyo anastahili pongezi kubwa.

Acha ujumbe