Kocha wa klabu ya Newcastle United Eddie Howe amewataka mashabiki wa klabu hiyo kua wavumilivu kwa kiungo mpya aliyesajiliwa klabuni hapo dirisha kubwa lililopita Sandro Tonali raia wa kimataifa wa Italia.

Kocha Eddie Howe anaamini kwenye ubora wa Sandro Tonali na kusema ni mchezaji mwenye  ubora mkubwa, Lakini watu wanatakiwa kumpa mda ili kuweza kuonesha alichokua anakionesha ndani ya Ac Milan.sandro tonaliKiungo Sandro Tonali amejiunga na klabu ya Newcastle United kwenye dirisha kubwa lililopita akitokea klabu ya Ac Milan ya nchini Italia, Lakini bado hajaonesha cheche zake ndani ya klabu hiyo kongwe nchini Uingereza.

Nyota huyo ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa kwa gharama ndani ya kikosi cha Newcastle hivo presha ni kubwa kwa upande wake, Lakini wa klabu hiyo anajaribu kuwataka mashabiki kutompa presha kubwa kwakua anajua nu mchezaji mzuri na atafanya vizuri tu.sandro tonaliKocha Eddie Howe suala la Sandro Tonali kuonesha makali ndani ya timu hiyo halina shaka kabisa, Kwani anatambua ubora wa kiungo huyo raia wa kimataifa wa Italia na ni suala la muda tu mashabiki wa klabu ya Newcastle watamfurahia.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa