Arda Guler Hataki Kuondoka Madrid

Kiungo kinda wa kimataifa wa Uturuki anayekipiga ndani ya klabu ya Real Madrid Arda Guler ameripotiwa kua hana mpango wowote wa kuondoka ndani ya miamba hiyo ya soka nchini Hispania.

Taarifa kadhaa zilisambaa kua Arda Guler ana mpango wa kuomba kuondoka klabuni hapo kwa mkopo kwajili ya kutafuta timu ambayo atapata nafasi ya kucheza mara kwa mara tofauti na ndani ya klabu hiyo.ARDA GULERKiungo huyo mwenye miaka 18 tu amekua hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara ndani ya Real Madrid tofauti na ilivyokua ndani ya klabu yake ya zamani ya Fenerbahce, Lakini wakala wa mchezaji huyo amethibitisha kua kiungo huyo ahana mpango wa kuondoka ndani ya Bernabeu.

Wakala wake ameeleza akili ya mchezaji huyo ipo ndani ya klabu hiyo kuhakikisha anaisaidia kumaliza msimu vizuri na taarifa za kuomba kuondoka kwa mkopo ndani ya timu hiyo hazina ukweli wowote.ARDA GULERKumekua na ushindani mkubwa wa nafasi ndani ya klabu ya Real Madrid hivo kumuwilia vigumu kiungo Arda Guler kuingia moja kwa moja kikosini, Lakini kocha Ancelotti amekua akisisitiza kua kijana huyo bado ana umri mdogo wakati wake  unakuja na ataweza kufanya makubwa klabuni hapo.

Acha ujumbe