Klabu ya Liverpool imeponea chupuchupu katika dimba la Old Trafford mbele ya mashetani wekundu katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza ulipigwa jioni ya leo na kumalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili.
Mchezo huo ambao uliwakutanisha mahasimu wakubwa wa soka kutoka nchini Uingereza klabu ya Manchester United ambao walikua wenyeji wa mchezo wakiwakaribisha klabu ya Liverpool.Mchezo huo ulionekana wa kasi kuanzia dakika ya kwanza mpaka ya mwisho kila timu ikionekana kuliandama lango la mwenzake, Japokua majogoo wa Anfield walionekana kutawala mchezo zaidi na ndio walikua wakwanza kupata goli kupitia kwa Luiz Dias dakika 23 ya mchezo.
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa vijana wa Jurgen Klopp kua mbele kwa bao moja kwa bila kipindi cha pili kilianza kama kipindi cha kwanza kwa kasi ileile, Dakika ya 50 baada ya makosa ya beki Jarrel Quansah Man United wanasawazisha bao kupitia kwa nahodha wao Bruno Fernandes.
Mchezo ukiendelea kua wa kasi ya hali ya juu dakika ya 67 ya mchezo kijana mdogo Kobbie Mainoo anaiandikia Man United bao la pili mchezo ukiendelea kua wa kutafutana majogoo wa Anfield wakafanikiwa kupata mkwaju wa penati dakika ya 84 na kusawazisha boa kupitia kwa Mohamed Salah.Kutokana na matokeo yaliyopatikana leo Old Trafford ni kama Man United wameharibia sherehe Liverpool ya kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, Kwani wanawafanya Arsenal kuongoza kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa wote wakiwa na alama 71.