Ali Kamwe: Yanga Imekuwa Maarufu Dunia Nzima

OFISA Habari wa Klabu ya Yanga Ali Kamwe, amesema kuwa Kwa Sasa Dunia nzima imeshaijua klabu ya Yanga kutokana na kile ambacho kimetokea wiki iliyopita kwenye mchezo wao dhidi ya Mamelodi Sundowns. Odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni njia rahisi ya kukupa mtonyo mrefu. Ingia mchezoni hapa.

 

Yanga

 

Kamwe ameenda mbali Kwa kuandika kuwa, TV na vyombo mbalimbali vya habari duniani vinalijadili goli lao lililokataliwa, huku akiwachapa baadhi ya wachambuzi walioibeza Yanga kabla ya Mechi zao mbili na Mamelodi.

“Na Umaarufu Tumeupata kweli kudadadeki. Dunia nzima inatujadili na kutafuta viclip vya kubishania kwamba Ni GOLI au SIO GOLI.

“Baadhi ya Vichambuzi Uchwara hapa Bongo vilivyosema Yanga Tunapigwa Nje Ndani na Mamelodi Visura vimewashuka saiv kwa Aibu.

Sasa hivi Wanasutana Wenyewe kwa Wenyewe kwenye vipindi vyao. Hii ndio Yanga na MWENYEKITI HUWA SIZUNGUMZI POROJO.

“Niliwaambia Hizi Game za Robo Fainali DUNIA ITATUJUA YANGA NI KINA NANI. Niwaambie Wananchi. Hamna Haja Yakubishana na watu wa hovyo, Huu sio muda wake. Tusiwape Kiki za bure bure MABONGOM. Let’s Focus kwenye Mechi yetu ya DODOMA JIJI na zitakazofata za LIGI KUU. Burudani iendeleee,” Ameandika Kamwe kwenye Instagram yake.

Jisajili na Meridianbet upate bonasi za kasino kibao na odds kubwa za ubashiri kwa machaguo kibao.

Acha ujumbe