Klabu ya Manchester United leo itakipiga katika mchezo wa nusu fainali wa kombe la Fa nchini Uingereza huku ikiwa na majeruhi kibao kwenye kikosi chake haswa eneo la ulinzi.
Manchester United leo itacheza mchezo huo huku mabeki wake wa katikati wakiwa wameumia wote na beki pekee wa katikati akiwa ni nahodha wa zamani wa klabu hiyo Harry Maguire.Mabeki wa kati wa klabu hiyo kama Raphael Varane, Lisandro Martinez, Johnny Evans, pamoja na kinda Willy Kambwala wote wanasumbuliwa na majeraha na hawatakua sehemu ya kikosi cha Man United leo kitakacjokipiga dhidi ya Conventry.
Klabu ya Manchester United imekua ikiandamwa na majeraha sana msimu huu huku mpaka sasa wachezaji wawili tu ndio hawajapata majeraha ndani ya kikosi hicho ambao ni nahodha Bruno Fernandes na golikipa namba moja wa klabu hiyo Andre Onana.Kuelekea mchezo wa leo inaelezwa kiungo wa ulinzi wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Brazil Casemiro ndio atacheza nafasi ya beki wa kati akishirikiana na Harry Maguire, Hii ikisababishwa na majeraha ambayo mabeki wa klabu hiyo wamekua wakiyapata mfululizo.