Azam Fc Watoa Thank You kwa Wanne

Klabu ya Azam Fc imetoa mkono wa kwaheri kwa wachezaji wake wanne ambao walikua wanaitumikia klabu hiyo msimu uliomalizika na wengine walikua kwa mkopo vilabu vingine.

Azam Fc wameachana na wachezaji kama Ayoub Reuben Lyanga, Charles Edward Manyama, Issa Ndala, pamoja na Malickou Ndoye hawa wachezaji watakua sio sehemu ya kikosi cha matajiri hao wa jiji la Dar-es-salaam kuelekea msimu wa 2024/25.azam fcKuelekea msimu ujao matajiri hao kutoka Chamazi wameelezwa kutaka kufanya usajili wa nguvu ambao utawapa nafasi ya kufanya vizuri katika ligi kuu ya NBC, Lakini pia kufanya vizuri kimataifa kwani msimu ujao watacheza ligi ya mabingwa barani Afrika hivo hawataki kutia aibu kabisa.

Azam Fc inapanga kufanya maboresho makubwa sana katika kikosi chake kuelekea msimu ujao ushindani ambao wameutoa kwenye ligi ya NBC msimu uliomalizika na kumaliza nafasi ya pili hawajaridhidshwa nao, Kwani kwa msimu ujao wanaamini kama wataboresha kikosi chao basi wanaweza kutwaa ubingwa wa ligi kuu.

Acha ujumbe