Nacho Kutimkia Saudia

Baada ya kudumu kwa miaka 23 ndani ya klabu ya Real Madrid aliyekua nahodha wa timu hiyo Nacho Fernandez ataondoka klabuni hapo na kutimkia ligi kuu ya Saudia Arabia.

Nacho Fernandez atajiunga na klabu ya Al- Qadsiah ambayo inashiriki ligi kuu nchini Saudia Arabia ambapo atasaini mkataba wa miaka miwili mpaka mwezi Juni mwaka 2026, Huku akiondoka ndani ya viunga vya Santiago Bernabeu kwa uhamisho huru kwkaua alimaliza mkataba na timu hiyo.nachoBeki huyo ambaye anaondoka ndnai ya klabu hiyo kama gwiji alihitajika na vilabu kadhaa barani ulaya lakini kwa upande wake alieleza wazi kwa ulaya ni Real Madrid tu, Hivo akaamua kuchagua kuelekea nchini Saudia Arabia ambapo atamaliza soka lake nchini humo.

Mchezaji huyo pia hakutaka kubaki barani ulaya kwakua hakutaka kucheza dhidi ya klabu yake ya Real Madrid ambayo ameitumikia kwa miaka 23 toka akiwa kijana mdogo akipita kwenye akademi ya klabu hiyo maarufu kama La Fabrica, Yote hayo ni mapenzi makubwa ambayo anayo dhidi ya klabu ya Real Madrid mabingwa wa ulaya.

Beki Nacho Fernandez anaondoka ndani ya Real Madrid akiwa mchezaji ambaye ametwaa mataji mengi zaidi ndani ya klabu hiyo sambamba na Luca Modric ambapo kwa pamoja wametwaa mataji 26 kila mmoja, Lakini pia beki huyo anaingia kwenye ile rekodi ya wachezaji waliotwaa matji mengi zaidi ya ulaya akiwa na mataji sita.

Acha ujumbe