Barkley Amalizana na Aston Villa

Kiungo wa klabu ya Luton Town ambayo imeshuka daraja Ross Barkley anakaribia kumalizana na klabu ya Aston Villa ili kukipiga katika klabu hiyo kuelekea msimu wa 2024/25.

Ross Barkley alikua moja ya viungo mahiri sana ndani ya klabu ya Luton Town jambo ambalo limemfanya kutolewa macho na vilabu vingi kwenye dirisha hili la usajili ukiachana na klabu ya Aston Villa, Lakini wababe hao kuoka Villa Park mpaka sasa ndio wanaelezwa wanakaribia kumsajili kiungo huyo.BarkleyAda ya uhamisho ya kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza inatajwa kua kiasi cha £5 milioni tu ambacho Aston Villa watapaswa kulipa kwa klabu ya Luton Town ambao watacheza Championship msimu ujao kwani walishindwa kubaki katika ligi kuu ya Uingereza msimu ujao.

Kiungo huyo wa zamani wa vilabu vya Chelsea na Everton amecheza kwa ubora mkubwa sana ndani ya klabu ya Luton sehemu pekee ambayo unaweza kusema alionesha ubora wake kama aliouonesha ndani ya Everton kipindi ambacho ndio anachipukia ndani ya viunga vya Goodson’s Park.BarkleySiku kadhaa mbele klabu ya Aston Villa itaweza kumtangaza Ross Barkley kama mchezaji wao mpya kuelekea msimu ujao kwani kila kitu wameshamalizana, Villa wamehakikisha wanafanya usajili wa kiungo mapema kwani kiungo wao wa kimataifa wa Brazil Douglas Luiz atatimka klabuni hapo kuelekea Juventus.

Acha ujumbe