Kwa mujibu wa chanzo Makini kutoka ndani ya Yanga kimeiambia Meridian Sports kuwa klabu ya Yanga imefanikiwa kupata Saini ya kipa wa Singida Fountain Gate Aboubakar Khomein.
Yanga wamemchukua Khomein kuwa mbadala wa Metacha Mnata ambaye amejiunga na Singida Black Stars.
Ingawa chanzo hicho kimesisitiza kuwa zimebaki taratibu kadhaa za kisheria kukamilisha uhamisho wake na rasmi awe mchezaji wa timu hiyo.
Yanga wanaelezwa kua wamehitaji kupata golikipa mwingine kutokana na golikipa wake namba mbili Abubakar Mshery inaelezwa ana mpango wa kutimka ndani ya klabu hiyo, Hivo klabu hiyo ikahitaji golikipa mwingine wa kuziba nafasi ya Mshery ndio sababu ya Khomein kujiunga na Wananchi.