Juventus Yamtaka Calafiori

Klabu ya Juventus inaelezwa kumuhitaji beki wa klabu ya Bologna raia wa kimataifa wa Italia Riccardo Calafiori ambaye anaiwakilisha timu ya taifa ya Italia kwenye michuano ya Euro mwaka huu.

Juventus ambayo imempa kazi kocha Thiago Motta ndani ya timu hiyo na tayari wameshaanza maboresho ya haraka katika kikosi hicho kwa kumsajili Douglas Luiz, Hivo kumuongeza beki huyo kwenye kikosi ni moja ya vipaumbele vyao kwa msimu huu.JuventusKuhitajika kwa Calafiori ndani ya klabu hiyo kunaelezwa kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na ushawishi wa kocha wa klabu hiyo Thiago Motta, Kwani kocha huyo amefanikiwa kufanya kazi na beki huyo msimu uliomalizika akiwa katika klabu ya Bologna.

Beki Riccardo Calafiori ni moja ya mabeki wanaozungumzwa kwasasa barani ulaya kutokana na umahiri wake mkubwa katika nafasi anayocheza, Hivo klabu ya Juventus kama watafanikiwa kunasa saini ya beki huyo ni wazi watakua wamepata moja ya wachezaji bora kabisa kwenye eneo la ulinzi kwasasa.

Acha ujumbe