Ashley Young Aongeza Mkataba Everton

Beki wa klabu ya Everton raia wa kimataifa wa Uingereza Ashley Young amefanikiwa kuongeza mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo ambao utamueka klabuni hapo mwaka 2025.

Ashley Young ambaye amekua klabuni hapo kwa misimu takribani miwili sasa akitokea klabu yake ya zamani ya Aston Villa amekubali kuendelea kubaki kwenye viunga vya Goodson’s Park na kuendelea kuitumikia klabu hiyo mpaka mwezi Juni 2025.ashley youngBeki huyo mkongwe ameongezewa mkataba ndani ya klabu hiyo kutokana na ubora ambao amekua nao tangu ajiunge na klabu ya Everton mwaka 2022, Hivo uongozi wa klabu hiyo umekubali kumuongezea mkataba mkongwe huyo aendelee kusalia ndani ya klabu hiyo.

Klabu ya Everton inamuona beki Ashley Young kama mchezaji ambaye anaweza kuendelea kuimarisha ubora wa kikosi hicho msimu ujao, Lakini pia kua sehemu ya uongozi ndani ya klabu hiyo kwani mchezaji huyo tayari ni mtu ambaye ana uzoefu mkubwa tofauti na wachezaji wengi ndani ya kikosi cha Everton.

Acha ujumbe