Joselu Atimkia Saudia

Mshambuliaji wa kimataifa ya Hispania Joselu Mato ambaye alikua anakipiga ndani ya klabu ya Real Madrid kwa mkopo akitokea Espanyol Joselu Mato ameamua kutimkia nchini Saudia Arabia.

Joselu Mato ameitumikia klabu ya Real Madrid kwa msimu mmoja akitokea klabu ya Espanyol lakini ilionekana kwamba anaweza kusaini mkataba wa kudumu ndani ya mabingwa hao wa ulaya, Mchezaji huyo ameamua kutimkia ligi kuu ya Saudia Arabia maarufu kama Saudian Pro League.joseluMshambuliaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Al Gharafa kutoka nchini Saudia ambapo atadumu ndani ya timu hiyo mpaka mwaka 2026, Lakini kukiwa na kipengele cha kuongeza mkataba wa mwaka mmoja baada ya miaka hiyo miwili kumalizika.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania ambaye kwasasa anaitumikia timu ya taifa ya Hispania kwenye michuano ya Euro 2024 ameamua kuungana na mchezaji mwenzake wa klabu ya Real Madrid Nacho Fernandez ambaye ametimka ndani ya timu na kuelekea nchini Saudia Arabia.joseluMshambuliaji Joselu Mato amekua mchezaji mwenye bahati sana kwani kwa mkopo wa mkataba wa mwaka mmoja ndani ya Real Madrid akitokea Espanyol amefanikiwa kutwaa mataji yasiyopungua matatu akianza na Spanish Super Cup, kombe la La liga, pamoja na taji la ligi ya mabingwa ulaya.

Acha ujumbe