Rafael Leao Haendi Popote

Mkurugenzi mkuu wa klabu ya Ac Milan Furlani ameweka wazi winga wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Ureno Rafael Leao hawezi kuondoka ndani ya klabu hiyo katika dirisha hili.

Winga Rafael Leao siku za hivi karibuni amekua akihusishwa na klabu ya Barcelona kutoka nchini Hispania kitu ambacho mkurugenzi huyo wa Ac Milan amekanusha vikali, Mchezaji huyo amekua mtu muhimu ndani ya klabu ya Ac Milan kwa misimu mitatu sasa hivo sio rahisi kumuachia kirahisi.rafael leao

Rafael Leão HATAONDOKA AC Milan msimu huu wa kiangazi.”

“Kuhamia Barcelona? Hakuna nafasi. Haiwezekani. Hataondoka kwenye klabu. Asilimia 100%.”

“Iwapo Rafa ataomba kuondoka? Hataomba kuondoka kwenye klabu.”

“Nadhani ujumbe wangu uko wazi kabisa, sivyo?

Haya ni maneno ambayo yametoka kwa mkurugenzi juu ya winga huyo wa kimtaifa wa Ureno kuhusishwa na Barcelona jambo ambalo kwasasa halitawezekana, Kwani mchezaji huyo ana mkataba na Ac Milan lakini pia kiwango cha pesa ambacho kitahitajika kuvunja mkataba wake Barcelona hawataweza kutoa kiasi hicho kwasasa.

Acha ujumbe