YANGA KUWAFANYA NGAZI VITAL 'O AZAM COMPLEX

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika wanahitaji ushindi mkubwa dhidi ya Vital’O ili kutuma salamu kwa wapinzani wao Afrika.

Agosti 24 Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa marudio.YANGAAli Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amebainisha kwamba wanatambua umuhimu wa mchezo huo licha ya kupata ushindi kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

“Mchezo wetu wa marudio dhidi ya Vital’O tunauchukua katika umuhimu na tunahitaji kupata ushindi mkubwa kwani inawezekana na wachezaji wapo tayari. Ushindi uliopita haina maana kwamba kazi imekwisha hapana tunakwenda kutafuta ushindi kwenye mchezo wetu wa marudiano.

“Katika mechi hizi za kimataifa kila baada ya mchezo mmoja kukamilika mchezo unaofuata ugumu wake huwa unakuwa mkubwa zaidi hilo tunalitambua, mashabiki ni muda wao kuendelea kununua tiketi kwa sasa kwa kuwa zipo na zinapatikana.”

Miongoni mwa wachezaji waliopo ndani ya kikosi cha Yanga ni Pacome, Aziz, Chama, Dube na Jonas Mkude, Clement Mzize, Dickson Job.

Acha ujumbe