Yanga Yambania Mzize Kwenda Wydad

Klabu ya Yanga imekataa ofa ya klabu ya Wydad Casablanca kutoka nchini Morocco ambayo inamuhitaji mshambuliaji wa klabu hiyo Clement Mzize.

Wydad wametuma ofa dola za kimarekani laki moja kwa klabu ya Yanga ambayo ni kiasi kinachokaribia milioni 280 lakini Uongozi wa mabingwa hao wa NBC hawaoni kama hiyo ni thamani hali ya mchezaji huyo ambaye kwasasa anafanya vizuri ndani ya kikosi hicho chini ya kocha Miguel Gamondi.yangaWananchi wameweka ngumu kwa Wydad Casablanca ambapo wanahitaji kiwango cha pesa kiongezeka kama kweli miamba hiyo ya soka kutoka nchini Morocco inamuhitaji Mzize, Kwani klabu hiyo inaamini thamani ya mshambuliaji huyo ni zaidi ya mamilioni hivo wao wanaelezwa kutoka angalau bilioni.

Mshambuliaji Clement Mzize inaelezwa yuko tayari kujiunga na klabu ya Wydad Casablanca lakini ambao wameweka ugumu ni klabu ya Yanga ambapo wanadai ofa waliyotoa Wydad haiendani na thamani ya mchezaji wao, Wydad wanaelezwa kufikiria kupandisha ofa yao mpaka kufikia dola za kimarekani laki nne.

Acha ujumbe