Aston Villa Yamuongezea Mkataba Martinez

Klabu ya Aston Villa imemuongezea mkataba golikipa wake namba moja raia wa kimataifa wa Argentina Emiliano Martinez ambapo mkataba huo utamuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2029.

Golikipa Emiliano Martinez inaelezwa amekubaliana na vipengele ambavyo Aston Villa wameviweka kwenye mkataba na kumfanya kusaini mkataba huo ambao utamuweka ndani ya viunga vya Villa Park kwa muda mrefu, Mkataba wa golikipa huyo namba moja wa Argentina unaambatana na maslahi kuongezeka pia.aston VillaKlabu ya Aston Villa miaka ya hivi karibuni inapambana sana kua klabu shindani katika ligi kuu ya Uingereza na hii ni kutokana na sajili ambazo wanazifanya ndani ya timu hiyo, Lakini pia kubakiza wachezaji wake muhimu ndani ya timu ambao walitarajiwa kuondoka ndani ya timu hiyo kwa miaka kadhaa iliyopita.

Golikipa Emiliano Martinez amekua moja ya magolikipa bora kwasasa duniani na hiyo ni kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha ndani ya klabu yake na timu ya taifa ya Argentina, Hivo kupewa kwake mkataba mpya sio suala la kushtua sana kwnai anastahili kutokana na kazi kubwa ambayo amekua akiifanya.

 

 

Acha ujumbe