Manuel Neuer, Thomas Muller Watundika Daluga Ujerumani

Golikipa na aliyekua nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani Manuel Neuer pamoja na mshambuliaji Thomas Muller wametangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Ujerumani.

Manuel Neuer na Muller wote baada ya kuitumikia timu ya taifa ya Ujerumani kwa muda mrefu na kwa mafanikio wamefikia uamuzi wa kuachana na timu hiyo, magwiji hao wamecheza michuano ya mwisho na timu ya taifa ya Ujerumani ilipigwa Ujerumani ya Euro 2024.manuel neuerMagwiji hao wamefanya makubwa kwenye soka la Ujerumani kuanzia vilabu vyao mpaka timu ya taifa ya nchi hiyo hivo wanaondoka kama wachezaji wenye heshima kubwa kuwahi kuvaa jezi ya timu ya taifa ya Ujerumani kwa takribani miaka kumi ambayo wameitumikia timu hiyo.

Wachezaji Thomas Muller, na Manuel Neuer wote walikua kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani ambacho kilitwaa taji la kombe la dunia mwaka 2014 katika ardhi ya Brazil, Hii ni heshima kubwa ambayo magwiji hao wameipata na wanaingia kwenye vitabu vya historia kama magwiji wa soka wa taifa hilo.

Acha ujumbe