Nahodha wa klabu ya Bayern Mnunich Manuel Neuer ambaye alikua akisumbuliwa na majeraha ya muda mrefu imearifiwa atarejea kuitumikia timu hiyo rasmi katika mchezo wa ligi kuu ya Ujerumani hapo kesho.
Manuel Neuer atarejea kesho katika mchezo wa ligi kuu ya Ujerumani dhidi ya klabu ya Darmstadt ambapo inaelezwa ataanza katika mchezo huo na taarifa ya kurejea kwake imetolewa na kocha klabu hiyo Thomas Tuchel.Golikipa huyo ambaye amekosekana kwa takribani mwaka mmoja sasa langoni mwa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani kutokana na majeraha aliyoyapata katika ajali aliyoipata mwaka jana mwishoni.
Klabu ya Bayern Munich ilipitia kipindi kigumu wakati wa majeraha ya nahodha wake huyo kutokana na mbadala wake kua changamoto,Kwani wote waliocheza nafasi yake wakati akiwa hayupo hawakufanikiwa kuvaa viatu vyake ipasavyo.Golikipa Yann Sommer aliyesajiliwa katika majira ya baridi mwezi Januari mwaka huu kwajili ya kuvaa viatu vya gwiji huyo tayari ameshatimkia nchini Italia katika klabu ya Inter Milan, Hivo Manuel Neuer anarejea klabuni hapo moja kwa moja na kwenda kukaa langoni kwenye nafasi yake.