Zaniolo Kikaangoni Baada ya Tonali

Kiungo wa klabu ya Aston Villa raia wa kimataifa wa Italia Nicolo Zaniolo ameingia kikaangoni baada ya kuitwa kwenye mahojiano kwenye ofisi ya mpelelezi wa serikali jijini Turin.

Nicolo Zaniolo anahusishwa na skendo ya kubashiri na sasa anachunguzwa na mamlaka zinazohusika nchini Italia katika jiji la Turin, Mchezaji huyo akikutwa na hatia anaweza kukumbwa na rungu la kutojihusisha na mpira.zanioloKiungo mwingine wa kimataifa wa Italia Sandro Tonali ambaye alikumbana na rungu la kutojihusisha na soka kwa muda wa miezi kumi kutokana na kuthibitika kujihusisha na michezo ya kamari.

Kiungo huyo wa Aston Villa alikua kundi moja na Sandro Tonali ambaye tayari ameshahukumiwa mpaka wakati huu, Hivo na kiungo huyo wa kimataifa wa Italia kama itathibitika kua amejihusisha na michezo hiyo ni wazi atakumbana na adhabu kali kama ya mwenzake Sandro Tonali.zanioloKlabu ya Aston Villa ina uwezekano wa kumkosa mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia, Kwani Zaniolo anaweza akukumbana na adhabu hiyo kwakua ni mara chache sana wachezaji wanaliohusishwa na michezo hiyo wanaepuka adhabu hiyo uchunguzi ukishafanyika.

 

Acha ujumbe