Zaniolo Atua Aston Villa

Kiungo wa zamani wa As Roma ambaye alikua anakipiga klabu ya Galatasaray Nicolo Zaniolo amefanikiwa kujiunga na klabu ya Aston Villa ya nchini Uingereza.

Nicolo Zaniolo amejiunga na Aston Villa kwa kiasi cha euro milioni 27 ikijumuisha na bonasi, Hivo kiungo huyo wa kimataifa wa Italia atasafiri kuelekea nchini Uingereza kwajili ya kufanya vipimo vya afya.zanioloTaarifa zinaeleza kua kiungo huyo alikua ana ndoto za kucheza kwenye ligi kuu ya Uingereza, Hivo ni wazi kucheza kwake ndani ya klabu ya Aston Villa itakua ni ndoto iliyokamilika.

Klabu ya Aston Villa licha ya kupoteza mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Newcastle United, Lakini ni moja ya vilabu ambavyo vimefanya usajili mzuri na mkubwa katika dirisha la usajili msimu huu.zanioloKiungo Nicolo Zaniolo ni miongoni mwa wachezaji waliokua wanafatiliwa kwa karibu na kocha wa klabu hiyo Unai Emery, Hivo kusajiliwa kwa kiungo huyo ni pendekezo la kocha wa klabu hiyo na anatarajiwa kuongeza kitu kikubwa klabuni hapo.

Acha ujumbe