Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag ameonekana kua na matumaini makubwa na mshambuliaji wake raia wa kimataifa wa Uingereza Marcus Rashford ambaye amekua chini ya kiwnago hivi karibuni.

Kocha Ten Hag anaamini njia pekee ya kumrudisha Marcus Rashford kwenye ubora wake ni kumpa nafasi ya kutosha katika michezo mingi kitu ambacho anaendelea kukifanya mpaka sasa.ten hagMshambuliaji Marcus Rashford amekua chini ya ubora wake hivi karibuni kwa kushindwa kua na kiwango bora ndani ya klabu ya Manchester United mpaka sasa akiwa na goli moja tu kwenye ligi kuu ya Uingereza.

Mshambuliaji huyo alikua kwenye ubora mkubwa msimu uliomalizika akifanikiwa kufunga mabao 30, Lakini msimu huu bado hajafanikiwa kuonesha cheche ambazo alifanikiwa kuonesha msimu uliomalizika.ten hagKocha Ten Hag anasema kwasasa anampa Rashford dakika za kutosha na mchezaji huyo anamaliza karibia kila hii ni kuhakikisha anamrudishia hali ya kujiamini mchezaji huyo na kurudi kufunga mabao mengi kama msimu uliomalizika


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa