Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag ameweka kua hahusiki juu ya suala la umiliki wa klabu hiyo kwa namna yeyote na akili yake yeye inawaza kuhusiana na timu yake tu.
Kocha Ten Hag aliulizwa juu ya tajiri Sir Jim Ratcliffe kununua umiliki wa 25% na kocha huyo ameweka wazi akili yake haipo kwa yanayoendelea nje ya uwanja zaidi yeye anaangalia zaidi timu yake na michezo inayofuata.Inafahamika klabu ya Manchester United ipo kwenye mchakato wa kuuzwa na wanunuaji walikua wawili na mpaka sasa amebakia mmoja, Ambapo mmoja amejitoa kutokana na kushindwana wamiliki wa sasa Familia ya Glazers.
Kocha huyo amesema suala la Sir Jim kuchukua asilimia 25 za ununuzi wa klabu hiyo linawahusu watu wa uongozi, Lakini yeye yupo makini kuangalia namna gani anaweza kuipatia matokeo katika michezo ijayo.Kocha Ten Hag anafikiria zaidi mchezo wao unaofuata wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Sheffield United utakaopigwa kesho katika dimba la Bramall Lane, Wakitazamia kupata matokeo ya ushindi kama walivyofanya katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Brentford.