Mchezo wa African Footbal League (AFL) kati ya klabu ya Simba ambao walikua wenyeji dhidi ya wageni klabu ya Al Ahly umemalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili.

Mchezo huo ambao umekua wa uzinduzi wa michuano hiyo mipya barani Afrika umeisha kwa timu zote kutoshana nguvu ya mabao mawili kwa mawili mbele ya umati wa mashabiki 6000,0 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.simbaMchezo huu ulianza ukiwa hauna kasi kubwa lakini baadae Al Ahly walifanikiwa kuukamata mchezo kwa kiwango kikubwa mbele ya wenyeji, Ambapo dakika ya 45 kipindi cha kwanza wakipata bao la uongozi kupitia kwa Reda Slim na mcheza kwenda mapumziko kwa Ahly kuongoza kwa bao moja kwa bila.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo Wekundu wa Msimbazi wenyeji wa mchezo wakihitaji kusawazisha bao ambalo wametanguliwa, Kasi yao ilifanikiwa pale dakika ya 53 ambapo Kibu Denis alisawazisha bao na kufanya ubao kusoma bao moja kwa moja.

Simba waliendeleza msako ambapo haikuchukua dakika 10 kupaa bao la uongozi ambapo dakika ya 59 Sadio Kanoute aliwapa Wekundu wa Msimbazi uongozi na kufanya ubao kusoma mabao mawili kwa Mnyama, Lakini bao hilo halikudumu kwani dakika ya 63 Mahamoud Khahraba akaiswazashia Al Alhy na matokeo kua mabao mawili kwa mawili.simbaMchezo huo mkali umemalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili ambapo Al Ahly wakiwa na faida ya mabao mawili ya ugenini, Huku mchezo wa marudiano ukipigwa nchini Misri wiki kadhaa zijazo ambapo Wekundu wa Msimbazi wakihitaji ushindi wa aina yeyote ili kufuzu hatua inayofuata.JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa