Ten Hag Hahofii Kibarua Chake

Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag ameeleza haogopi kibarua chake kua matatani licha ya kupoteza mchezo wa pili wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu ya Galatasaray jana usiku.

Erik Ten Hag anakiri kua wanapitia kipindi kigumu lakini kwake haoni hatari yeyote kwa kibarua chake, Kwani anaamini timu ipo pamoja na wanapambana pamoja kuanzia wachezaji, jopo la makocha na uongozi pia wa klabu hiyo.ten hagKlabu ya Manchester United ipo kwenye hatari kubwa kwasasa kwani ina matokeo mabaya sana, Ambapo mpaka sasa wameshapoteza michezo sita kwenye michuano yote ambapo kwenye ligi ya mabingwa ulaya wamepoteza michezo miwili ya awali.

Manchester United kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo wanapoteza michezo miwili ya kwanza katika ligi ya mabingwa ulaya na mpaka wakati huu wanashika mkia kwenye kundi lao mpaka sasa wakiwa hawana alama hata moja.ten hagKocha Erik Ten Hag anasema anajua wako kwenye hali mbaya na hawapo kwenye ubora wao, Lakini akisema wanapaswa kufanya vizuri zaidi na kinachotakiwa ni kuweza kubadilika lakini wakati huohuo anajiamini kwenye kibarua chake kwakua uongozi unampa ushirikiano.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.