Hispania,Morocco na Ureno Kuandaa Kombe la Dunia 2030

Mataifa matatu Hispania, Ureno na Morocco wanatarajia kuandaa michuano ya kombe la dunia mwaka 2030 baada ya kushinda kinyang’anyiro hicho na kutangazwa na kama waandaji rasmi.

Mataifa ya Hispania, Ureno, na Morocco walituma maombi ya kuandaa michuano hiyo mwaka 2030 kwa shirikisho la soka duniani FIFA na wamefanikiwa, Kwani wamepitishwa rasmi kama waandaji wa michuano hiyo mwaka 2030.hispaniaMataifa hayo inafahamika kijiografia hawapo mbalimbali licha ya nchini moja kutoka bara tofauti ambayo ni Morocco, Lakini nchi zingine mbili zilizobaki zinatokea barani ulaya na ikielezwa sababnu kubwa ya wao kujiunga pamoja kutaka kuandaa michuano hiyo ni ukaribu uliopo baina ya mataifa hayo.

Hili litakwenda kua kombe la dunia la kwanza kuchezwa katika mabara matatu kwani nchi tatu ambazo zinaandaa michuano hiyo mbili zinatoka bara la ulaya ambazo ni Hispania na Ureno Huku Morocco wao wakitoka bara la Afrika, Lakini pia timu za Argentina, Uruguay na Paraguay zitacheza michezo yao ya awali nyumbani.hispaniaMataifa ya Paraguay, Uruguay na Argentina itacheza michezo yao ya awali katika ardhi za nyumbani hii ikitokana na mataifa hayo kusherekea miaka 100 tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo kwa mara ya kwanza, Ambapo ilipigwa nchini Uruguay mwaka 1930.

 

Acha ujumbe