KOCHA wa Simba Roberto Oliviera (Robertinho) amesema kuwa kwenye mechi ya kesho dhidi ya Tanzania Prisons watacheza mpira safi kama ambao walikuwa wanahitaji mashabiki wao.
Robertinho aliweka wazi kuwa anajua kuna ugumu kwenye mechi hiyo lakini watafanya kila kitu ili kuweza kupata ushindi na kubwa ni kuwafanya mashabiki wake kufurahia mpira mzuri.Robertinho alisema: “Tunaenda kucheza soka safi pamoja na kushinda, tunawaheshimu Tanzania Prison na tuna kumbukumbu msimu uliopita walitupa mechi ngumu.
“Lakini tumejipanga, sisi tutaingia uwanjani kwa lengo la kucheza soka safi na kushinda. Najua mashabiki wanahitaji furaha na sisi tutawapa furaha, wapo waliosafiri kuja hapa Mbeya, hatutaki kuwaangusha.Simba watashuka dimbani Sokoine Mbeya kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu, kusaka alama tatu muhimu ili kujiweka sawa kwenye msimamo wa ligi.