KLABU ya Tanzania Prisons imesema makosa yaliyoonekana kwenye mechi tatu zilizopita yamefanyiwa kazi, hivyo Simba isitarajie mteremko, huku nyota wa timu hiyo wakipania pointi tatu kesho.
Prisons haijashinda mchezo wowote katika michezo mitatu iliyocheza ikivuna pointi moja na kubakia mkiani kwenye msimamo wa Ligi Kuu, huku Simba ikiwa ya tatu na alama zake tisa. Kocha mkuu wa timu hiyo, Fred Felix ‘Minziro’ alisema:“Tunahitaji ushindi pamoja na ugumu wa mchezo utakavyokuwa. Nimewaandaa vyema nyota wangu na nimewaelekeza kutofanya makosa yoyote ya kizembe”
“Tuko mkiani na hatujaonja ushindi hadi sasa baada ya kuanzia ugenini. Sasa tumekuja nyumbani hivyo lazima tuwape raha mashabiki na kujiweka pazuri kwenye msimamo”Nahodha wa Tanzania Prisons, Jumanne Elifadhili alisema wanafahamu Simba ina kikosi bora, hivyo watapambana na mchezaji mmoja