KOCHA mkuu wa Simba Mbrazili, Robert Olivieira (Robertinho) amewachimba mkwara mzito mastraika wa timu hiyo kuhakikisha wanarekebisha makosa yao ya kushindwa kutumia vizuri nafasi wanazotengeneza. Tumia vizuri machaguo mengi yaliyopo Meridianbet yenye odds kubwa kubeti mechi nyingi.
Simba kwa sasa wanaendelea na kambi ya maandalizi ya mchezo wao wa mkondo wa pili wa hatua ya pili ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos unaotarajiwa kupigwa siku ya Jumapili Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Dar es Salaam.
Ikumbukwe kuwa Simba wataingia katika mchezo huo wakiwa wameshuhudia matokeo ya sare mabao 2-2 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya Dynamos uliopigwa nchini Zambia.
Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.
Robertinho alisema: “Tumetoka kupata matokeo ya ushindi muhimu wa mchezo wetu dhidi ya Coastal Union, licha ya matokeo hayo lakini naweza kusema hatukuwa kwenye kiwango bora kwani tulipoteza nafasi sita mpaka saba za kufunga mabao.
“Kama tungezitumia basi zingetuwezesha kupata ushindi mnono, lakini huu ndio mpira wa miguu tunarudi nyumbani kujipanga na sitarajii kuona tunarudia makosa.”
Kikosi cha Simba kinatarajiwa kurejea mazoezini leo Jumatatu kujiandaa na mchezo huo dhidi ya Power Dynamos ya Zambia, mara baada ya kupewa mapumziko ya siku moja.
Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.