ROBERTINHO AWAPA MAJUKUMU MIQUISONNE NA ONANA

KOCHA Mkuu wa Simba Mbrazili, Roberto Oliviera ‘Robertinho‘ ataingia uwanjani kuwavaa wapinzani wao Power Dynamos na staili ya kipekee akiwapa majukumu viungo wake wa pembeni akiwemo Willy Onana na Luis Misquissone.

Robertinho ameamua kuingia na mbinu hiyo wakati wakiwa kwenye maandalizi ya kuivaa Dynamos kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao utapigwa nchini Zambia.ROBERTINHORobertinho alisema kuwa anataka kuona timu yake inatengeneza mabao kupitia pembeni na sio katikati pekee katika michezo ijayo.

Robertinho alisema kuwa katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu Bara timu yake, imepata mabao yao mengi ambayo yametokana na kati tofauti na pembeni ambapo wanacheza Luis, Onana, Kibu Denis, Aubin Kramo na Clatous Chama.

Aliongeza kuwa tayari amewapa mbinu nzuri za kupata mabao kupitia pembeni akiwatumia viungo na mabeki wa pembeni, Shomari Kapombe na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.

“Timu yangu katikati ipo vizuri ina viungo wengi wenye uwezo mkubwa wa kupitisha mipira kwa washambuliaji na kupata mabao.ROBERTINHO“Sitaki niendelee kutumia staili hiyo moja pekee ya kupata mabao, kwani nikikutana na timu inayoweza kuziba vizuri katikati, ngumu kupata ushindi.

“Hivyo nimeona ni bora nikawapa mbinu hiyo nyingine ya ushindi, kama hiyo ya katikati wapinzani wetu watatuzuia,” alisema Robertinho

Acha ujumbe